INDIA-USALAMA

India: Zaidi ya watu 60 waokolewa kutoka chini ya vifusi vya jengo

Visa vya majengo kuporomoka ni kawaida nchini India, kwa sababu ya kazi duni ya ujenzi, vifaa ambavyo havina ubora na kutoheshimu viwango vya ujenzi.
Visa vya majengo kuporomoka ni kawaida nchini India, kwa sababu ya kazi duni ya ujenzi, vifaa ambavyo havina ubora na kutoheshimu viwango vya ujenzi. REUTERS

Zaidi ya manusura 60 wameondolewa chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka katika mji wa viwanda karibu na mji mkuu wa India Bombay, afisa mwandamizi amesema, wakati timu za uokoaji zinaendelea na juhudi zao.

Matangazo ya kibiashara

Jengo la ghorofa tano, lililojengwa karibu na eneo lenye watu wenye maisha duni huko Mahad na ambapo wanaishi watu 200, liliporomoka Jumatatu jioni, mwakilishi wa polisi kwenye eneo la tukio amesema.

Kulingana na diwani mmoja kutoka mji wa Mahad, ambao ni kama kilomita 165 kutoka Bombay, "mtu mmoja alipoteza maisha na karibu wengine 30 bado wamekwama chini ya vifusi vya jengo."

Sababu ya ajali haijulikani. Lakini, visa vya majengo kuporomoka ni kawaida nchini India, kwa sababu ya kazi duni ya ujenzi, vifaa ambavyo havina ubora na kutoheshimu viwango vya ujenzi.

Kila mwaka kati ya mwezi Juni na Septemba, wakati wa msimu wa mvua, mvua kubwa husababisha kuporomoka kwa majengo yaliyojengwa kwa vifaa dhaifu.