URUSI-UJERUMANI-NAVALNY-USHIRIKIANO

Kesi ya Navalny yageuka kuwa mzozo wa kidiplomasia kati ya Berlin na Moscow

Maafisa wa polisi wakitoa katika hospitali ya Charité ambapo kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny anaendelea kuhudumiwa huko Berlin Agosti 22, 2020.
Maafisa wa polisi wakitoa katika hospitali ya Charité ambapo kiongozi wa upinzani wa Urusi Alexei Navalny anaendelea kuhudumiwa huko Berlin Agosti 22, 2020. REUTERS/Fabrizio Bensch

Masuali yameibuka iwapo mpinzani mkuu na mkosoaji mkubwa wa rais wa Urusi, Vladimiri Putin, Alexei Navalny alipewa sumu. Kwa upande wa madaktari wa Ujerumani wanaomtibu, wamesema kuna uwezekano kuwa Alexei Navalny amepewa sumu.

Matangazo ya kibiashara

Madaktari wa Urusi ambao walimchunguza hapo awali wanaendelea kupinga madai hayo.

Kwa sasa kesi hiyo imegeuka kuwa mzozo wa kidiplomasia. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezungumzia suala hiloakitoa wito kwa viongozi wa Urusi.

Katika taarifa, Kansela wa Ujerumani amewasihi viongozi wa Urusi "kusuluhisha suala hili mara moja, kwa undani zaidi na kwa uwazi." Angela Merkel pia ameomba wale waliohusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Angela Merkel alichapisha taarifa hii mara tu baada ya hospitali inayomtibu Alexeï Navalny kukamilisha uchunguzi wake.

Vipimo vilivyofanywa kwa mpinzani huyo nchini Urusi vinaonyesha dalili za sumu, madaktari wamesema. Inasemekana ni chembe la sumu linalofanana na lile ambalo alipewa afisa wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake miaka miwili iliyopita huko London.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 44 alisafirishwa Berlin Jumamosi kutokea Siberia, ambako alianza kuugua akiwa kwenye ndege katika kile madaktari wa Urusi walisema ni matatizo ya afya yake.

Mkosoaji huyo wa serikali ya Urusi, alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi Alhamisi baada ya ndege yake kutua kwa dharura katika mji wa Siberia wa Omsk. Navalny kwa sasa amepewa ulinzi wa serikali wakati akiendelea kutibiwa.