KOREA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Seoul yaagiza madaktari kusitisha mgomo

Korea Kusini inakabiliwa na moja ya milipuko mbaya zaidi wa janga la Corona.
Korea Kusini inakabiliwa na moja ya milipuko mbaya zaidi wa janga la Corona. REUTERS

Korea Kusini imewataka madaktari katika mji mkuu Seoul kusitisha mgomo wao na waweze kurejea kazini wakati ili kukabiliana na ugezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Wito huo unakuja wakati madaktari wanaanza mgomo wa siku tatu kupinga mapendekezo kadhaa ya serikali, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya madaktari kwa minajili ya kukabiliana na mgogoro wa kiafya unaosababishwa na ugonjwa hatari wa Covid-19.

Mgomo huu unatokea wakati Korea Kusini inakabiliwa na moja ya milipuko mbaya zaidi wa janga la Corona. Mamlaka ya afya imeripoti kesi mpya 320 zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita. Angalau kesi mpya zaidi ya mia moja zimeripotiwa kila siku kwa zaidi ya wiki moja.

"Serikali sasa haina chaguo jingine bali ni kuchukuwa tu hatua muhimu za kisheria zinazohitajika kwa kuepuka kuhatarisha maisha na usalama wa raia," Waziri wa Afya Park Neung-hoo amesema katika mkutano na vyombo vya habari.

Kwa hofu ya mlipuko mpya, serikali inataka kuongeza wanafunzi 4,000 wanaosomea udaktari katika miaka kumi ijayo.