INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 75,000 zathibitishwa India

India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa idadi ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil.
India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa idadi ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil. REUTERS

India imerekodi visa vipya 75,760 vya maambukizi ya virusi ya Corona vilivyothibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, ikiwa ni idadi kubwa ya maambukizi mapya kwa siku moja tangu kuzuka kwa janga hilo, kulingana na data iliyotolewa leo Alhamisi na Wizara ya Afya.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa India imerekodi zaidi ya visa milioni 3.31 vya maambukizi na vifo 60,472, ikiwa ni pamoja na vifo 1,023 vilivyoripotiwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita.

India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na ugonjwa huo kwa idadi ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil.

Kufikia sasa zaidi ya watu milioni 22 wameambukizwa virusi vya Corona ulimwenguni, kwa mujibu wa takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins, huku watu 788, 000 wakithibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.