URUSI-NAVALNY-UCHUNGUZI-USALAMA

Polisi ya Urusi yaanzisha uchunguzi baada ya Navalny kulazwa hospitalini

Navalny kwa sasa amepewa ulinzi wa serikali wakati akiendelea kutibiwa.
Navalny kwa sasa amepewa ulinzi wa serikali wakati akiendelea kutibiwa. REUTERS

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi imetangaza kuanzisha uchunguzi kuhusu sababu ya Alexey Navalny, kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais wa Urusi vladimir Putin, kulazwa hospitalini, shirika la habari la Tass limeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Alexey Navalny alilazwa hospitalini Alhamisi ya wiki iliyopita alipokuwa katika hali mbaya huko Omsk, Siberia, kisha kusafirishwa jijini Berlin, nchini ujerumani, siku mbili baadaye.

Wafuasi wake wanadai kuwa akipewa sumu, madai ambayo yamethibitishwa na madaktari wa Ujerumani. Hata hivyo madaktari wa hospitali ya Omsk, huko Siberia, walitupilia mbali madai hayo.

Katika taarifa, Kansela wa Ujerumani aliwasihi viongozi wa Urusi "kusuluhisha suala hili mara moja, kwa undani zaidi na kwa uwazi." Angela Merkel pia ameomba wale waliohusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Angela Merkel alichapisha taarifa hii mara tu baada ya hospitali inayomtibu Alexeï Navalny kukamilisha uchunguzi wake.

Vipimo vilivyofanywa kwa mpinzani huyo nchini Urusi vinaonyesha dalili ya chembe chembe za sumu, madaktari wamesema. Inasemekana ni chembe la sumu linalofanana na lile ambalo alipewa afisa wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na binti yake miaka miwili iliyopita huko London.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 44 alisafirishwa Berlin Jumamosi kutokea Siberia, ambako alianza kuugua akiwa kwenye ndege katika kile madaktari wa Urusi walisema ni matatizo ya afya yake.

Mkosoaji huyo wa serikali ya Urusi, alikimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi Alhamisi baada ya ndege yake kutua kwa dharura katika mji wa Siberia wa Omsk. Navalny kwa sasa amepewa ulinzi wa serikali wakati akiendelea kutibiwa.