URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya visa vya maambukizi yapindukia zaidi ya 980,000 Urusi

Sampuli za chanjo ya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020.
Sampuli za chanjo ya Corona iliyotengenezwa na Taasisi ya Utafiti ya Gamaleya, huko Moscow, Urusi, Agosti 6, 2020. The Russian Direct Investment Fund (RDIF)/Handout via REUTERS

Urusi imerekodi kesi mpya 4,829 za maambukizi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, na kufikisha jumla ya viisa 980,405 nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Urusi ambayo ni nchi ya nne iliyoathirika zaidi na janga hilo imerekodi vifo 110 katika muda wa saa 24 izilizopita, na kufikisha jumla ya vifo 16,914 nchini humo tangu kuzuka kwa kwa janga hilo.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Hivi karibuni shirika la afya Duniani, WHO, lilizitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona na kuonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.