URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yaongezeka hadi zaidi ya 17,000 nchini Urusi

Moscow, mji mku wa Urusi.
Moscow, mji mku wa Urusi. cattu/ Pixabay

Urusi imerekodi vifo vingine 111 vya maambukizi ya virusi vya Corona Jumamosi Agosti 29, na kufanya idadi ya watu waliokufa nchini humo kufikia 17,025.

Matangazo ya kibiashara

Pamoja na visa vipya 4,941, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona sasa imefikia 985,346, na kuifanya Urusi kuwa nchi ya nne iliyoathiriwa zaidi na janga hilo ulimwenguni, baada ra Marekani, Brazil, na India.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.