INDIA-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi ya Corona yaongezeka hadi milioni 3.6 India

kiwa na visa Milioni 3.62 kwa jumla, India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na janga la Covid-19 baada ya Marekani na Brazil.
kiwa na visa Milioni 3.62 kwa jumla, India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na janga la Covid-19 baada ya Marekani na Brazil. REUTERS

India imerekodi leo Jumatatu visa vipya 78,512 vya maambukizi ya virusi vya Corona, idadi iliyo karibu na ile iliyotangazwa Jumapili agosti 30. Idadi ya vifo pia imeongezeka.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili India iliripoti visa vipya 78,761, ongezeko kubwa la kila siku la idadi ya maambukizi ambayo hayajawahi kuripotiwa duniani tangu kuzuka kwa janga hilo.

Ikiwa na visa Milioni 3.62 kwa jumla, India ni nchi ya tatu iliyoathirika zaidi na janga la Covid-19 baada ya Marekani na Brazil lakini ripoti yake ya kila siku iko juu zaidi duniani tangu Agosti 7.

India pia imerekodi vifo vipya 971 leo Jumatatu, na kufanya jumla ya vifo kufikia 64,469, kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.