MAREKANI-TAIWAN-USHIRIKIANO

Marekani yaongeza usaidizi wake kwa Taiwan dhidi ya shinikizo kutoka Beijing

Marekani, kama nchi nyingi, haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan, lakini ndio msaidizi mkuu wa kisiwa hicho na muuzaji wa silaha.
Marekani, kama nchi nyingi, haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan, lakini ndio msaidizi mkuu wa kisiwa hicho na muuzaji wa silaha. REUTERS

Marekani imetangaza kwamba imeanzisha mazungumzo mapya ya pande mbili kuhusu na Taiwan, mpango ambao Washington imesema utaimarisha uhusiano na Taipei na kuunga mkono kisiwa hicho dhidi ya shinikizo kubwa kutoka Beijing.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Marekani pia umebaini kutangaza dhamana sita za usalama zilizotolewa kwa Taiwan wakati wa utawala wa Ronald Reagan, hatua ambayo wachambuzi wanaona njia ya ungwaji mkono zaidi kwa kisiwa hicho.

Tangazo hilo linakuja wakati kukiwa na shinikizo kubwa kutoka China dhidi ya Taiwan, ambayo inaichukulia kama mkoa ulioasi, na kuongeza mvutano kati ya Washington na Beijing kuhusu maswala yenye utata ya biashara, janga la Corona na Hong Kong.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ana matumaini ya kuchaguliwa tena katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Novemba, amechukuwa msimamo mkali dhidi ya China kuwa moja ya pointi zake muhimu za kampeni.

Afisa mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya nje amesema wakati wa mkutano ulioandaliwa na shirika la Conservative Heritage Foundation kwamba hatua ya hivi karibuni ya Marekani haikuwa na mabadiliko katika sera ya nje ya Washington lakini ilikuwa sehemu ya kifurushi cha " marekebisho muhimu ".

"Tutaendelea kusaidia Taiwan kupinga kampeni ya Chama cha Kikomunisti cha China ya kushinikiza, kufanya vitisho na kuitenga Taiwan," amesema David Stilwell, mwakilishi mkuu wa sera ya mambo ya nje ya Marekani katika ukanda wa Asia ya Mashariki.

Marekani, kama nchi nyingi, haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na Taiwan, lakini ndio msaidizi mkuu wa kisiwa hicho na muuzaji wa silaha.