UTURUKI-UGIRIKI-USALAMA-USHIRIKIANO

Uturuki kuendelea na shughuli zake katika Bahari ya Mediterania, Ugiriki yapandwa na hasira

Umoja wa Ulaya umebaini kwamba unaanda vikwazo dhidi ya Uturuki.
Umoja wa Ulaya umebaini kwamba unaanda vikwazo dhidi ya Uturuki. REUTERS

Uturuki imetangaza kuwa meli yake ya Oruc Reis itaendelea na utafiti katika eneo lenye mgogoro mashariki mwa Mediterania hadi Septemba 12. Uamuzi ambao umesababisha ugiriki kupandwa na hasira.

Matangazo ya kibiashara

Ugiriki imekiri kuwa eneo hilo ni sehemu yake na kuchukulia shuhguli hizo kama ni kinyume cha sheria.

Nchi hizo mbili, washirika wa Jumuiya ya Kujihalmi ya Nchi za Magharibi, NATO, zimefanya mazoezi ya kijeshi katika eneo hilo linalozuzaniwa, na kuonyesha hatari ya kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili.

Wakati meli ya Oruç Reis ikiendelea na utafiti, shughuli iliyotarajiwa kumalizika leo Jumanne, jeshi la wanamaji la Uturuki limetoa tangazo likisema meli ya Oruc Reis itaendelea na kazi yake hadi Septemba 12.

Tangazo hilo linakuja baada ya Umoja wa Ulaya kutoa wito wa mazungumzo na kuomba Ankara isichukue hatua za upande mmoja ambazo zinaweza kuzidisha uhasama katika eneo la Mashariki ya Mediterania.

Umoja wa Ulaya umebaini kwamba unaanda vikwazo dhidi ya Uturuki.

Wizara ya Mambo ya nje ya Ugiriki imeliita tangazo hilo la Uturuki kuwa kinyume cha sheria na kuitaka nchi hiyo jirani kutuliza mvutano na kushirikiana katika kuleta utulivu wa kikanda.

"Uturuki inaendelea kupuuzia wito wa mazungumzo na kuongeza chokochoko," Wizara ya Mambo ya nje ya Ugiriki imesema katika taarifa.