JAPAN-ABE-SIASA-USALAMA

Suga atangaza nia yake ya kuwania kwenye nafasi ya kiongozi wa PLD

Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya Japani, Yoshihide Suga, anayepewa nafasi kubwa ya kuwa waziri mkuu mpya nchini Japan
Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya Japani, Yoshihide Suga, anayepewa nafasi kubwa ya kuwa waziri mkuu mpya nchini Japan REUTERS

Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya Japani, Yoshihide Suga, anayepewa nafasi kubwa ya kuwa waziri mkuu mpya nchini Japan, ametangaza rasmi nia yake ya kuwania kwenye nafasi ya uongozi wa chama tawala cha Liberal Democratic Party (PLD).

Matangazo ya kibiashara

"Nimeamua kuwania kwenye nafasi ya uongoz wa uchama cha PLD baada ya Shinzo Abe kujiuzulu," amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

PLD inatarajia kumteua mrithi wa Shinzo Abe, ambaye alitangaza kujiuzulu kwenye wadhifa wake siku ya Ijumaa kutokana na sababu za kiafya, kupitia utaratibu uliorahisishwa, Septemba 14.

Jumanne wiki hii, Waziri wa zamani wa Ulinzi Shigeru Ishiba na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje Fumio Kishida walitangaza nia yao ya kuwania kwenye nafasi ya uongozi wa chama cha PLD.

Waziri wa Mambo ya nje wa sasa, Toshimitsu Motegi, amesema bado hajachukua uamuzi. Waziri wa Ulinzi Taro Kono kwa upande wake ameamua kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho, kulingana na shirika la habari la Kyodo News.