URUSI-NAVALNY-UCHUNGUZI-USALAMA

Moscow yataka kufanya mazungumzo na Berlin ili kupata taarifa zaidi kuhusu Navalny

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Moscow inataka kufanya mazungumzo na Ujerumani ili kuelewa ni kitu gani kilichosababisha Navalny analazwa hospitalini.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Moscow inataka kufanya mazungumzo na Ujerumani ili kuelewa ni kitu gani kilichosababisha Navalny analazwa hospitalini. Mladen ANTONOV / AFP

Kremlin imeitolea wito Ujerumani kwa mazungumzo ili kupata taarifa zaidi juu ya madai ya sumu aliyopewa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexeï Navalny, aambaye amelazwa hospitalini Berlin baada ya kuwa katika hali ya mahututi nchini Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Jumatano wiki hii Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema ana vithibitisho kwamba Navalny alipewa sumu aina ya Novichok, ambayo tayari ilitumiwa dhidi ya afisa wa zamani wa upelelezi wa Urusi Sergei Skripal mwaka 2018 nchini Uingereza.

Mamlaka nchini Urusi yimekanusha shutma hizo dhidi yake. Kwa sasa, imeanzisha tu ukaguzi wa awali kuhusu kesi hiyo, bila hata hivyo kufungua uchunguzi.

Akilaumu madaktari wa Ujerumani kwa ukosefu wao wa uwazi, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema Moscow inataka kufanya mazungumzo na Ujerumani ili kuelewa ni kitu gani kilichosababisha Navalny analazwa hospitalini. Ameongeza kuwa wataalamu wa Urusi wanakichunguza kesi hiyo.

"Kulingana na toleo la madaktari wetu, haikuwa sumu," amesema Dmitry Peskov. "Wataalam wa Ujerumani wameweza kutambua aina fulani ya sumu. Tunategemea kukutana kwa mazungumzo na wenzetu wa Ujerumani."

"Uchunguzi unafanywa na wataalam wetu na ikiwa kuna uthibitisho wa uwepo wa vitu vyenye sumu katika nyenzo za kibaolojia za mgonjwa, ni wazi kutakuwa na athari za kisheria. Tunamwomba mtu yeyote kuleta ushahidi, " msemaji wa Kremlin ameongeza.

Mahakama ya Urusi imetupilia mbali malalamiko yaliyowasilishwa na wafuasi wa Navalny dhidi ya kile wanachokiona kama "kutowajibika" kwa Kamati ya Upelelezi, chombo kinachohusika nakushughulikia uhalifu mkubwa. Wamekuwa wakidai tangu Agosti 20 kufunguliwa kwa uchunguzi wa jaribio la mauaji.