URUSI-UJERUMANI-NAVALNY-USHIRIKIANO

Alexei Navalny aanza kupata fahamu baada ya kuwa katika hali ya mahututi kwa siku kadhaa

Hospitali ya Charité Mitte huko Berin, ambapo kiongozi wa upinzani Urusi Alexeï Navalny amelazwa, Agosti 22, 2020.
Hospitali ya Charité Mitte huko Berin, ambapo kiongozi wa upinzani Urusi Alexeï Navalny amelazwa, Agosti 22, 2020. REUTERS/Fabrizio Bensch

Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexeï Navalny "ameanza kupata fahamu" siku chache baada ya kuwa katika hali ya mahututi ", kulinga na taarifa kutoka hospitali moja ya Berlin anakopewa huduma ya matibabu.

Matangazo ya kibiashara

Alexeï Navalny ataanza kusitisha kutumia mashine ya kupumulia, , taarifa hiyo imeongeza.

Alexeï Navalny "kuna ishara anazofanya wakati unazungumza naye", hospitali ya Charité mjini Berlin, ambapo mkosoaji huyo wa Vladimir Putin anapewa huduma ya matibabu tangu Agosti 22, baada ya kupewa sumu aina Novichok.

Katika taarifa yake, hata hivyo, hospitali hiyo imeonya kuwa ni "mapema mno kutathmini athari za sumu yake kali aliyopewa."

Awali Kremlin imeliita jaribio la "upuuzi" na "lisilokubalika" na "kuihusisha Urusi kwa njia yoyote na kile kilichotokea" dhidi ya Alexei Navalny.

Berlin yatoa muda wa mwisho

Kauli hiyo inakuja wakati wito wa kuichukulia vikwazo Urusi unazidi kuongezeka katika nchi za Magharibi: Berlin imetoa muda wa mwisho wa siku chache wa kupokea maelezo kutoka Moscow, na athari kwa mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 pia zinatathminiwa.