CHINA-CORONA-AFYA

China: Chanjo ya Corona yaweza kuwa tayari mwezi Novemba

Majaribio ya kliniki ya "awamu ya 3" yanaenda vizuri na chanjo zinaweza kuwa tayari kwa raia mwezi Novemba au Desemba, Guizhen Wu amesema kwenye mahojiano kwenye runinga ya serikali.
Majaribio ya kliniki ya "awamu ya 3" yanaenda vizuri na chanjo zinaweza kuwa tayari kwa raia mwezi Novemba au Desemba, Guizhen Wu amesema kwenye mahojiano kwenye runinga ya serikali. REUTERS

Chanjo dhidi ya Corona zinazoendelea kutengenezwa hivi sasa nchini China zinaweza kupatikana kwa umma mapema mwezi Novemba, Guizhen Wu, mwakilishi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini China amesema.

Matangazo ya kibiashara

Aina nne ya chanjo zinazotengenezwa nchini China zimeingia katika hatua ya mwisho ya majaribio ya kliniki.

Vipimo vya angalau chanjo tatu za majaribio vimependekezwa kwa wafanyakazi muhimu kama sehemu ya mpango wa dharura uliozinduliwa mwezi Julai.

Majaribio ya kliniki ya "awamu ya 3" yanaenda vizuri na chanjo zinaweza kuwa tayari kwa raia mwezi Novemba au Desemba, Guizhen Wu amesema kwenye mahojiano kwenye runinga ya serikali.

Amesema yeye mwenyewe alipata chanjo ya majaribio mwezi Aprili, bila kutaja ni ipi, na akaongeza kuwa hakuwa na dalili zozote zisizo za kawaida katika miezi ya hivi karibuni.