BELARUS-NAVALNY-SIASA-USALAMA

Maabara Ufaransa na Uswisi: Alexeï Navalny alipewa sumu

Alexei Navalny, kiongozi wa upinzani nchini Urusi na mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin.
Alexei Navalny, kiongozi wa upinzani nchini Urusi na mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin. REUTERS/Tatyana Makeyeva

Maabara nchini Ufaransa na Uswisi zimethibitisha kuwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexeï Navalny alipewa sumu. Madai ambayo serikali ya Belarus imeendelea kukanusha.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, msemaji wa kansela Angela Merkel, Steffen Seibert amesema matokeo ya maabara nchini Ufaransa na Uswisi sasa yanathibitisha ushahidi wa Ujerumani kuhusu Navalny ambaye ameendelea kupata matibabu nchini humo.

Haya yanajiri wakati rais wa Belarus, Jumatatu wiki hii Alexander Lukashenko alizuru Urusi na kukutana  na rais Vladmir Putin kutafuta uungwaji mkono wa serikali ya Urusi baada ya kuendelea kushuhudiwa kwa maandamano makubwa ya umma nchini mwake.

Putin amesema Urusi itatoa mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.5 kwa Belarus na kutimiza majukumu yake chini ya mkataba wa umoja kati ya nchi hizo jirani. Putin pia amempongeza Lukashenko kwa ahadi yake ya kufanya mageuzi ya katiba.

Hata hivyo upinzani umepuzilia mbali mazungumzo ya Lukashenko kuhusu mageuzi ya katiba wakisema ni njama tu ya kutuliza hasira za waandamanaji.

Upinzani nchini Belarus unamshtumu Lukashenko kwa wizi wa kura katika uchaguzi urais uliyofayika mwezi uliopita . Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza Alexander Lukashenko kwamba alishinda kiti cha urais kwa asililmia 80 ya kura zote zilizohesabiwa.