INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: India yavuka kizingiti cha maambukizi Milioni tano

Huko Kolkata, India, maafisa wa afya wakishiriki gwarise, huku wakivalia mavazi maalumu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru. Kuenea kwa janga hili katika nchi hii yenye watu wengi kunatia wasiwasi wataalam we
Huko Kolkata, India, maafisa wa afya wakishiriki gwarise, huku wakivalia mavazi maalumu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru. Kuenea kwa janga hili katika nchi hii yenye watu wengi kunatia wasiwasi wataalam we Dibyangshu SARKAR / AFP

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini India imevuka kizingiti cha milioni 5, baada ya visa vipya 90,123 kuthibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatano na Wizara ya Afya.

Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliofariki dunia imeongezeka hadi 82,066, baada ya vifo vipya 1,290 kuripotiwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita.

Mapema wiki hii shirika la Afya Duniani, WHO, lilisema vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona, vinatarajiwa kuongeka kati ya mwezi Oktoba na Novemba.

Mwakilishi wa WHO barani Ulaya Hans Kluge alitoa onyo hilo, licha ya kusema kuwa hivi karibuni, bara hilo limeshuhudia ongezeko la maambukizi lakini idadi ya vifo haijaongezeka sana.

Aidha, Kluge alionya kuwa hata iwapo chanjo itapatikana, haitakuwa mwisho wa maambukizi hayo.

Bara la Ulaya lina maambukizi zaidi ya Milioni Mbili na vifo zaidi ya Laki Mbili.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.