INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 97,800 zathibitishwa nchini India, rekodi ya kila siku

India ni nchi ya pili ulimwenguni iliyoathirika zaidi na mgogoro huu wa kiafya kwa idadi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani.
India ni nchi ya pili ulimwenguni iliyoathirika zaidi na mgogoro huu wa kiafya kwa idadi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani. REUTERS

India imerekodi kesi mpya 97,894 zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, rekodi ya kila siku tangu kuzuka kwa janga hilo, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na Wizara ya Afya ya India.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa watu milioni 5.12 wameambukizwa virusi vya Corona nchini India, kulingana na takwimu za serikali, ambayo pia imethibitisha vifo vipya 1,132 kwa siku moja kwa jumla ya vifo 83,198.

Angalau vifo 1,000 vimerekodiwa kila siku nchini India katika wiki mbili zilizopita.

India ni nchi ya pili ulimwenguni iliyoathirika zaidi na mgogoro huu wa kiafya kwa idadi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.