URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Urusi yathibitisha karibu visa 6,000 vya maambukizi mapya

Urusi inaendelea kuathirika na ugonjwa hatari wa COVID-19.
Urusi inaendelea kuathirika na ugonjwa hatari wa COVID-19. REUTERS

Urusi, nchi ya nne iliyoathirika zaidi na ugonjwa hatari wa Corona kwa upande wa maambukizi, imerekodi leo Ijumaa visa vipya 5,905 vya maambukizi, na kufikisha jumla ya watu 1,091,186 walioambukizwa virusi hivyo.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka za afya nchini Urusi pia zimethibitisha vifo vpiya 134 katika muda wa saa 24zilizopita. Idadi ya watu walmiofariki dunia kutokana na virusi hivyo ya Corona, imefikia sasa iko 19,195.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.