EU-MAREKANI-BELARUS-SIASA

Umoja wa Ulaya: Lukashenko sio rais halali wa Belarus

Rais wa Belarus amlianza rasmi muhula wake wa sita Jumatano, Septemba 23, baada ya sherehe ya kuapishwa ambayo haikutangazwa kabla.
Rais wa Belarus amlianza rasmi muhula wake wa sita Jumatano, Septemba 23, baada ya sherehe ya kuapishwa ambayo haikutangazwa kabla. Reuters

Umoja wa Ulaya haumtambui Alexander Lukashenko kama rais halali wa Belarus, Mkuu wa sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amesema siku moja baada ya kuapishwa kwa rais wa Belarus.

Matangazo ya kibiashara

"Umoja wa Ulaya unasema kuwa uchaguzi wa urais wa Agosti 9 nchini Belarus haukuwa huru na wa haki. Umoja wa Ulaya hautambui matokeo yake ya uwongo," Josep Borrell amesema katika taarifa.

"Kutokana na hali, madai ya kutawazwa kwa Alexander Lukashenko Septemba 23, 2020 na muhula wake mpya anaodai havina uhalali wa kidemokrasia", Josep Borrell amebaini, huku akiongeza kuwa madai haya ya kuapishwa "yanapingana moja kwa moja na matakwa ya sehemu kubwa ya raia wa Belarus ".

"Msimamo wa Umoja wa Ulaya uko wazi: Raia wa Belarus wanastahili haki ya kuwakilishwa na wale watakaowachagua kwa uhuru kupitia uchaguzi mpya ulio wazi, na wa kuaminika."

Msimamo wa Umoja wa Ulaya unakuja baada ya Washington kutangaza msimamo kama huo siku ya Jumatano ikibaini kwamba haimchulii Lukashenko kama rais wa Belarus aliyechaguliwa kihalali.

Alexander Lukashenko ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1994, alitawazwa Jumatano wiki kwa muhula mpya kama rais wa Belarus katika hafla ya kuapishwa iliyopingwa na upinzani, ambao umeingia mitaani.