INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 86,000 za maambukizi zathibitishwa India

India ni nchi ya pili ulimwenguni iliyoathirika zaidi na mgogoro huu wa kiafya kwa idadi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani.
India ni nchi ya pili ulimwenguni iliyoathirika zaidi na mgogoro huu wa kiafya kwa idadi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani. REUTERS

India imerekodi visa vipya 86,052 vya maambukizi ya virusi vya Corona uchafuzi katika muda wa saa ishirini na nnezilizopita, kulingana na takwimu zilizotolewa na Wizara ya Afya ya india leo Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa india ina visa milioni 5.82 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 92,290, baada ya vifo 1,141 kuthibitishwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita.

Angalau vifo 1,000 vilirekodiwa kila siku nchini India katika wiki tatu zilizopita.

India ni nchi ya pili ulimwenguni iliyoathirika zaidi na mgogoro huu wa kiafya kwa idadi ya visa vya maambukizi, baada ya Marekani.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.