UKRAINE-AJALI

Ishirini na mbili wafariki dunia katika ajali ya ndege ya jeshi la Ukraine

Ndege hiyo ilikuwa katika zoezi la mafunzo, rais Volodimir Zelenski amesema.
Ndege hiyo ilikuwa katika zoezi la mafunzo, rais Volodimir Zelenski amesema. REUTERS

Ndege ya usafiri ya jeshi la Ukraine iliyokuwa ikiabiri watu 28 ilianguka Ijumaa jioni kaskazini mashariki mwa Ukraine. Angalau watu 22 wamlifariki dunia, mamlaka imesema.

Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilikuwa imebeba marubani wa wanafunzi wa chuo cha jeshi la wanaanga, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema

Watu wawili walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya, awizara hiyo imeongeza.

"Miili ya watu 22 imepatikana, watu wawili wamejeruhiwa na zoezi la kutafuta watu wengine wanne linaendelea," mamlaka ya hali za dharura imebaini.

Ndege hiyo ilikuwa katika zoezi la mafunzo, rais Volodimir Zelenski amesema.