BELARUS-MACRON-SIASA-USALAMA

Macron: Ni wazi Lukashenko lazima aondoke

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, tarehe 23 Septemba 2020 huko Kiev.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, tarehe 23 Septemba 2020 huko Kiev. AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema katika mahojiano na Gazeti la Le Journal du dimanche kwamba rais wa Belarus Alexander Lukashneko 'anapaswa kuachia ngazi.'

Matangazo ya kibiashara

"Kinachondelea Belarus ni mgogoro wa kiutawala, utawala wa kimabavu ambao hauwezi kukubali mtazamo wa kidemokrasia na ambao ukpo kwa kutumia nguvu. Ni wazi kwamba Lukashenko lazima aondoke", amesema rais wa Ufaransa, ambaye amenukuliwa na Gazeti la Le Journal du dimanche.

Rais wa Ufaransa pia amesema "anavutiwa na ujasiri wa waandamanaji" nchini Belarus. "Wanajua hatari wanazochukua kwa kuandamana kila mwishoni mwa wiki na bado, wanaendelea na maandamano ya kutaka kukomaza demokrasia katika nchi hii ambayo demokrasia imeminywa kwa muda mrefu," ameongeza raisMacron, ambaye ameongeza kwamba "wanawake" hasa, ambao wanaandamana kila Jumamosi, wanastahili kupewa heshima kubwa".

Zaidi ya watu 90, wengi wao wakiwa wanawake, walikamatwa Jumamosi wakati wa mikusanyiko ya upinzani, shirika moja lisilo la kiserikali limesema.

Kuhusu jukumu la rais wa Urusi Vladimir Putin katika kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa baada ya uchaguzi wa rais Lukashenko Agosti 9, unaoendelea kupingwa, Bw. Macron amesema kuwa jitihada hizo za Putin bado ni ndoto.

"Nilipozungumza na Vladimir Putin Septemba 14, siku ambayo alimpokea Lukashenko huko Sochi. Nilimwambia kwamba Urusi ina jukumu katika hali inayoendelea Belarus, na jukumu hilo linaweza kuwa chanya ikiwa atamshawishi Lukashenko kukubalimatokeo ya uchaguzi na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa. Ni wiki mbili sas zimepita, jambo hilo halijafanyika, "amesema rais wa Ufaransa, aliyenukuliwa na gazeti la Le Journal du dimanche.

Emmanuel Macron atafanya ziara yake ya kwanza Lithuania na Latvia kuanzia Jumatatu hadi Jumatano, nchi mbili za Baltic ambazo ana imani kuwa zitasaidia katika mgogoro huo wa kisiasa nchini Belarus na shinikizo la Urusi.

Umoja wa Ulaya na nchi za Baltic hazijatambua uchaguzi wa Lukashenko na Lithuania inaendelea kumpa hifadhi ya ukimbizi kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tikhanovskaïa.