URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 8,000 vya maambukizi vyaripotiwa Urusi

Mamlaka pia imeripoti vifo vipya 61 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufikisha idadi rasmi ya vifo kufikia 20,385.
Mamlaka pia imeripoti vifo vipya 61 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufikisha idadi rasmi ya vifo kufikia 20,385. REUTERS/Tatyana Makeyeva

Urusi imerekodi visa vipya 8,135 vya maambukizi ya virusi vya Corona, ikiwa ni idadi kubwa tangu Juni 16, wakati nchi hiyo imethibitisha juma ya visa 1,159,573 vya maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka pia imeripoti vifo vipya 61 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufikisha idadi rasmi ya vifo kufikia 20,385.

 

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.