BELARUSUFARANSA-USALAMA-SIASA

Kiongozi wa upinzani Belarus amtaka Macron kuwa 'mpatanishi'

Svetlana Tikhanovskaya na Maria Kolesnikova, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, Agosti 10. S. Tikhanovskaïa, kiongozi mkuu wa upinzani, akimtaka rais anayemaliza muda wake A. Loukachenko, 'kuachia madaraka'.
Svetlana Tikhanovskaya na Maria Kolesnikova, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumatatu hii, Agosti 10. S. Tikhanovskaïa, kiongozi mkuu wa upinzani, akimtaka rais anayemaliza muda wake A. Loukachenko, 'kuachia madaraka'. Sergei GAPON / AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Svetlana Tikhanovskaya ametoa wito kwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuwa "mpatanishi ambaye tunahitaji sana" kusuluhisha mgogoro nchini Belarus. Ameyasema hayo katika mahojiano na shirika la habari la AFP Jumatatu wiki huko Vilnius, ambapo rais wa Ufaransa amezuru leo mchana.

Matangazo ya kibiashara

"Tunahitaji mtu anyeweza kusha kusuluhisha ili kuzuia damu zaidi isimwagike. Bwana Macron anaweza kuwa mpatanishi, pamoja na viongozi wa nchi zingine. Anaweza kumshawishi Bwana Putin, ambaye ana uhusiano naye mzuri, "amesema Tikhanovskaïa, ambaye anatarajia kukutana na rais wa Ufaransa Jumanne wiki hii wakati wa ziara yake huko Vilnius.

"Tumeomba mkutano huu lakini bado hatuna uthibitisho. Lakini natumai tunaweza kukutana naye, labda kesho" (Jumanne), ameongeza. Mkutano huu wa kwanza na kiongozi wa kimataifa kwa mujibu wa kiongozi wa upinzani nchini Belarus "uthibitisho muhimu".

"Bwana Macron na Ufaransa wanajulikana kuwa wamepatanisha katika visa vingine vingi. Kwa kweli tunapendelea kutatua mgogoro huu sisi wenyewe lakini tunaona kuwa ukatili unaendelea, na raia wa Belarui wanateseka na kwamba mamlaka yetu haitilii manani mazungumzo ".

"Bwana Macron ni mmoja wa viongozi wenye nguvu barani Ulaya na ulimwenguni na anaweza kuwa angalau mmoja wa wapatanishi," amebaini.