ARMENIA-AZERBAIJAN-USALAMA

Mapigano yaendelea Nagorno-Karabakh, kumi na tano wauawa

Hali ya wasiwasi ilianza kushuhudiwa kati ya Armenia na Azerbaijan Jumapili asubuhi baada ya Armenia kudai kuwa wanajeshi wa Azerbaijan na kuwauwa raia, ambao idadi yao haikutajwa.
Hali ya wasiwasi ilianza kushuhudiwa kati ya Armenia na Azerbaijan Jumapili asubuhi baada ya Armenia kudai kuwa wanajeshi wa Azerbaijan na kuwauwa raia, ambao idadi yao haikutajwa. REUTERS

Mapigano yamendelea leo Jumatatu asubuhi kati ya vikosi vya Armenia na Azerbaijan katika mkoa uliojitenga wa Nagorno-Karabakh, ambapo mamlaka zimetangaza kupoteza wapiganaji 15 wengine kwa kila upande.

Matangazo ya kibiashara

Huko Yerevan, Wizara ya Ulinzi ya Armenia imesema mapigano hayajasimama usiku kucha.

Huko Baku, Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan imebaini kwamba vikosi vya Armenia wimekuwa winatekeleza mashambulizi ya mji wa Tartar.

Siku ya Jumapili nchi ya Armenia ilitangaza matumizi ya sheria za kijeshi nchini humo baada ya kutokea kwa makabiliano makali kati ya jeshi lake na waasi katika jimbo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh, kati ya nchi hiyo na Azerbaijan.

Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri Mkuu Nikol Pashinyan kupitia ukurasa wake wa Facebook, baada ya rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, kuapa kulishinda jeshi la Armenia.

Hali ya wasiwasi ilianza kushuhudiwa kati ya Armenia na Azerbaijan Jumapili asubuhi baada ya Armenia kudai kuwa wanajeshi wa Azerbaijan na kuwauwa raia, ambao idadi yao haikutajwa.

Tangu mwaka 1991, nchi hizo mbili zimekuwa zikipambania jimbo la Nagorno-Karabakh lililojitangazia uhuru wake kutoka ka Umoja wa Kisoviet.