BELARUS-UFARANSA-SIASA-USALAMA

Macron kusaidia kuachiliwa huru kwa wapinzani nchini Belarus

Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tsikhanouskaya.
Kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tsikhanouskaya. REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kusaidia ili kufanyika kwa mazungumzo nchini Belarus na kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tsikhanouskaya amesema baada ya mkutano na rais wa Ufaransa nchini Lithuania.

Matangazo ya kibiashara

"Ametuahidi kufanya atachoweza kusaidia kufanyika kwa mazungumzo katika mgogoro wa kisiasa ambao nchi yetu unapitia. Amesema itabidi mchakato huo wende haraka kwa sababu watu wengi wanateseka kwa kutokana na utawala, watu wengi wako gerezani, na atafanya kila awezalo kusaidia kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa kisiasa, ”Svetlana Tsikhanouskaya amewaambia waandishi wa habari.

Svetlana Tsikhanouskaya alitoroka nchi yake baada ya uchaguzi wa Agosti 9 ambao Rais anayemaliza muda wake Alexander Lukashenko alitangazwa mshindi, hali ambayo imesababisha maandamano makubwa nchini humo, maandamano yanayoendelea kuzimwa kwa nguvu za kupita kiasia na mamlaka.

Emmanuel Macron anafanya ziara yake ya kwanza Lithuania na Latvia tangu Jumatatu wiki hii hadi Jumatano, nchi mbili za Baltic ambazo ana imani kuwa zitasaidia katika mgogoro huo wa kisiasa nchini Belarus na shinikizo la Urusi.

Umoja wa Ulaya na nchi za Baltic hazijatambua uchaguzi wa Lukashenko na Lithuania inaendelea kumpa hifadhi ya ukimbizi kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tikhanovskaïa.

Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.