ARMENIA-AZERBAIJAN-USALAMA

Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan yaripotiwa nje ya Nagorno-Karabakh

Mataifa mbalimbali duniani, yakiongozwa na Marekani, Urusi, Iran na Mataifa ya Ulaya, yametaka pande zote mbili kuacha makabiliano na kuanza mazungumzo.
Mataifa mbalimbali duniani, yakiongozwa na Marekani, Urusi, Iran na Mataifa ya Ulaya, yametaka pande zote mbili kuacha makabiliano na kuanza mazungumzo. KAREN MINASYAN / AFP

Armenia na Azabajani zimelaumiana Jumanne kwa kufyatua risasi kwenye ngome za mbali katika eneo la Nagorno-Karabakh ambapo mapigano yanaendelea kwa siku ya tatu mfululizo, na kusababisha majeruhi zaidi upande wa raia.

Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumapili, mapigano yamesababisha vifo kadhaa katika eneo hili llililojitenga la Azerbaijan, lakini mpaigano hayo yamesambaa kwenye mipaka kati ya nchi hizo mbili.

Kulingana na maafisa wa Armenia, silaha za kivita za adui na shambulio la ndege isiy kuwa na rubani vimesababisha kifo cha mtu mmoja huko Vardenis, eneo la Armenia lililoko karibu kilomita ishirini kutoka mpakani.

Wakati huo huo wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imebaini kwamba jeshi la Armenia limefanya shambulizi katika eneo la Dacheskan kutoka Vardenis, madai ambayo yamekanushwa na Yerevan.

Akinukuliwa na shirika la habari la Interfax, Rais Ilham Aliev amebaini kwamba watu kumi, raia wa Azebaijan, wameuawa tangu Jumapili.

Mataifa mbalimbali duniani, yakiongozwa na Marekani, Urusi, Iran na Mataifa ya Ulaya, yametaka pande zote mbili kuacha makabiliano na kuanza mazungumzo.

Tangu mwaka 1991, nchi hizo mbili zimekuwa zikipambania jimbo la Nagorno-Karabakh lililojitangazia uhuru wake kutoka ka Umoja wa Kisoviet.