BELARUS-UFARANSA-SIASA-USALAMA

Rais wa Ufaransa kukutana na kiongozi wa upinzani Belarus

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya rais huko Vilnius, Lithuania.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya rais huko Vilnius, Lithuania. Ludovic MARIN / AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema yuko tayar kukutana na kiongozi wa upinzani nchini Belarus, Svetlana Tikhanovskaya, ambaye awali alimtaka rais Macron kuwa mpatanishi katika mzozo unaoshuhudiwa nchini mwake.

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Belarus imekuwa katika hali ya mvurugano tangu maamndamano kuzuka mwezi uliopita baada ya Tikhanovsakaya kupoteza katika uchaguzi wa Agosti 9 ambao rais Alexander Lukashenko alidai kushinda licha ya madai ya wizi kura.

Aidha, Tikhanovsakaya ametaka Umoja wa Ulaya kuziwekea vikwazo vya bishara nchi zinazounga mkono serikali ya rais Alexander Lukashenko.

Emmanuel Macron anafanya ziara yake ya kwanza Lithuania na Latvia tangu Jumatatu wiki hii hadi Jumatano, nchi mbili za Baltic ambazo ana imani kuwa zitasaidia katika mgogoro huo wa kisiasa nchini Belarus na shinikizo la Urusi.

Umoja wa Ulaya na nchi za Baltic hazijatambua uchaguzi wa Lukashenko na Lithuania inaendelea kumpa hifadhi ya ukimbizi kiongozi wa upinzani nchini Belarus Svetlana Tikhanovskaïa.

Belarus haikuwahi kuwa nchi ya pekee hadi karne ya 20. Maeneo yake yalikuwa chini ya himaya mbalimbali kama vile Poland, Lithuania na Urusi. Belarus ilikuwa kitengo cha Umoja wa Kisovyet tangu 1919/1922 hadi 1991.