CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 12 vya maambukizi vyathibitishwa China

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019. REUTERS

China imerekodi visa vipya 12 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita. Watu wote hao walipatikana na virusi vay Corona ni raia waliotokea katika nchi za kigeni, Mamlaka ya afya imesema leo Alhamisi katika katika mkutano wake wa kila siku kuhusu janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu hizi, jumla ya visa 85,415 vya maambukizi vimethibitishwa katika bara la China.

Janga la Corona limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa leo Alhamisi.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.