EU-BELARUS-CYPRUS-UCHUMI-USHIRIKIANO

EU yataka kuishawishi Cyprus idhinishe vikwazo dhidi ya Belarus

Brussels imeahidi kuchukuwa vikwazo dhidi ya Minsk baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 ambao serikali za Magharibi na upinzani nchini Belarus wanauona kuwa uligubikwa na udanganyifu.
Brussels imeahidi kuchukuwa vikwazo dhidi ya Minsk baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 ambao serikali za Magharibi na upinzani nchini Belarus wanauona kuwa uligubikwa na udanganyifu. REUTERS/Yves Herman

Wakuu wa nchi na serikali za Umoja wa Ulaya wanatarajia kujaribu kumaliza makubaliano juu ya suala la vikwazo dhidi ya Belarus kwa kumaliza mzozo ambao ni tofauti kuhusu Uturuki, hali ambayo imeongeza sintofahamu kwa umoja huo kwa kuchukuwa uamuzi wa pamoja.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wanaokutana jijini Brussels, mji mkuu wa Ubelgiji kwa mkutano wa siku mbili, watajaribu kuishawishi Cyprus, mmoja wa wanachama wadogo zaidi wa Umoja huo, ambao unatuhumiwa kuzuia azimio la kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Belarusi kutokana na uhasama tofauti na Uturuki ambayo imesababisha mvutano katika Mashariki ya Mediterania.

Brussels imeahidi kuchukuwa vikwazo dhidi ya Minsk baada ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 ambao serikali za Magharibi na upinzani nchini Belarus wanauona kuwa uligubikwa na udanganyifu.

Sintofahamu ya wiki za hivi karibuni imeharibu uaminifu wa Umoja wa Ulaya ambapo uamuzi unachukuliwa kwa maelewano, wanadiplomasia wamesema, wakati Uingereza na Canada zimeiwekea vikwazo Minsk ili kuonyesha uungwaji wao mkono kwa waandamanaji wanaotetea demokrasia.