URUSI-NAVALNY-SIASA-USALAMA

Navalny amtuhumu Putin kwa kuamuru apewe sumu

Alexeï Navalny, kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais wa Urusi Vladimir Putin.
Alexeï Navalny, kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais wa Urusi Vladimir Putin. Mladen ANTONOV / AFP

Kiongozi wa Urusi na mkosoaji mkubwa wa rais wa nchi hiyo Alexeï Navalny, anamtuhumu rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kujaribu kumuua kwa sumu, katika mahojiano na jarida la Ujerumani la Der Spiegel.

Matangazo ya kibiashara

Alexeï Navalny alilazwa hospitalini Agosti 20 baada ya kuwa katika hali mbaya huko Omsk, Siberia, na baadaye kusafirishwa siku mbili baadaye katika hospitali jijini Berlin, nchini Ujerumani. Serikali ya Ujerumani ilihitimisha kuwa alikuwa alipewa sumu ya Novichok inayoathiri "mishipa ya fahamu'. Sumu iliyetengenezwa na jeshi la Kisoviet mnamo miaka ya 1970 na 1980.

Serikali za Magharibi zinataka maelezo zaidi kutoka kwa serikali ya Urusi, ambayo inakanusha kuhusika kwa kitendo hicho na inasema kuwa haina uthibitisho kwamba kitendo hicho ni cha jinai.

Alexeï Navalny aliruhusiwa kuondoka hospitali jijini Berlin wiki moja iliyopita.

"Ninathibitisha kwamba Putin anahusika na uhalifu huu na sina maelezo mengine ya kile kilichotokea," Alexeï Navalny amesema katika sehemu ya mahojiano yanayotarajiwa kurushwa hewa leo Alhamisi.

Viongozi kutoka kote ulimwenguni walilaani tukio la kupewa sumu kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny katika jaribio la kutaka kumuuwa.