INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya maambukizi yapindukia Milioni 6.4 India

India imerekodi kesi mpya 81,484 zilizothibitishwa za maambukizi ya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kufanya jumla ya idadi ya visa vya maambukizi kufikia Milioni 6.4, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na Wizara ya Afya ya India.

Wizara ya Afya ya India imeripoti vifo vipya 1,095 vilivyotokana na janga hilo, na kufanya jumla ya idadi ya vifo kufikia 99,773.
Wizara ya Afya ya India imeripoti vifo vipya 1,095 vilivyotokana na janga hilo, na kufanya jumla ya idadi ya vifo kufikia 99,773. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, India inarekodi idadi kubwa zaidi ya visa vipya vya maambukizi ya kila siku duniani.

Wizara ya Afya pia imeripoti vifo vipya 1,095 vilivyotokana na janga hilo, na kufanya jumla ya idadi ya vifo kufikia 99,773.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.