BELARUS-EU-VIKWAZO-USHIRIKIANO

EU yauwekea vikwazo utawala wa Belarus na kuitishia Uturuki

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel katika mkutano wa EU huko Brussels, Oktoba 2, 2020.
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel katika mkutano wa EU huko Brussels, Oktoba 2, 2020. JOHANNA GERON / POOL / AFP

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya kuiwekea vikwazo serikali iliyoko madarakani nchini Belarus, lakini sio vikwazo hivyo havimlengi Rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Umoja wa Ulaya pia wamekubaliana juu ya ujumbe thabiti ulioambatana na vitisho vya vikwazo dhidi ya Uturuki, baada ya mazungumzo magumu.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokutana katika mkutano huko Brussels, wametoa idhini ya kuwawekea vikwazo waliohusika na ukandamizaji nchini Belarus. Vikwazo hivi vinahusu karibu maafisa 40 wa Belarus.

"Tumeamua kutekeleza vikwazo dhidi ya wale wote wanaohusika na ukandamizaji huko Belarus," rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Charles Michel, ametangaza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari na Rais wa Tume Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

Vikwazo hivi vitaanza kutumika "kuanzia Ijumaa" Oktoba 2, Charles Michel ameongeza.

Vikwazo hivi vilikuwa vimeombwa na upinzani nchini Belarus. "Hii inaweza kutusaidia sana", amesema kiongozi wa upinzani, Svetlana Tikhanovskaya, aliyekimbilia uhamishoni nchini Lithuania baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9.