INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya vifo 100,000 vyathibitishwa India

India imerekodi kesi mpya 81,484 zilizothibitishwa za maambukizi ya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kufanya jumla ya idadi ya visa vya maambukizi kufikia Milioni 6.4.
India imerekodi kesi mpya 81,484 zilizothibitishwa za maambukizi ya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kufanya jumla ya idadi ya visa vya maambukizi kufikia Milioni 6.4. Dibyangshu SARKAR / AFP

Idadi ya vifo vinavyohusiana na virusi vya coronavirus nchini India vimezidi 100,000 Jumamosi hii, Oktoba 3, kulingana na takwimu rasmi, na kuifanya India kuwa nchi ya tatu kwa vifo baada ya Marekani na Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Jumla ya vifo 100,842 vimerekodiwa, kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya ya India. Janga hilo linaendelea kukithiri nchini India, nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu duniani.

India imerekodi kesi mpya 81,484 zilizothibitishwa za maambukizi ya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kufanya jumla ya idadi ya visa vya maambukizi kufikia Milioni 6.4, kulingana na takwimu zilizotolewa jana Ijumaa na Wizara ya Afya ya India.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.