URUSI-VYOMBO VYA HABARI-USALAMA

Mwandishi wa habari wa Urusi ajichoma moto Nizhny Novgorod

Moja ya mitaa katika mwa mji wa Nizhny Novgorod, Urusi, Julai 10, 2015.
Moja ya mitaa katika mwa mji wa Nizhny Novgorod, Urusi, Julai 10, 2015. REUTERS/Maxim Shemetov

Mwandishi wa habari wa Urusi mefariki dunia jana Ijumaa baada ya kuchoma moto nguo zake nje ya majengo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Urusi huko Nizhny Novgorod, siku moja baada ya polisi kufanya msako katika kwa nyumba yake, limeripoti gazeti ambalo alikuwa akifanya kazi.

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kujichoma moto, Irina Slavina aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook: "Niwaomba kuhusisha kifo changu kwa serikali ya Urusi."

Alikuwa mhariri mkuu wa Gazeti la Koza Press, maarufu kwamsimamo wake "Hakuna udhibiti. Hakuna agizo kutoka juu."

Mwandishi huyo wa habari alieleza kwenye Facebook Alhamisi kwamba maafisa wa polisi na maafisa wa uchunguzi walikuwa wamekuja nyumbani kwake kutafuta "nyaraka na akaunti" zinazohusiana na vuguvugu la "Open Russia", linaloofadhiliwa na kiongozi wa upinzani Mikhail Khodorkovsky.

Tume ya Upelelezi imetangaza kuanzisha uchunguzi wa awali.Mji wa Nizhny Novgorod, una idadi ya watu milioni 1.3, na unapatikana karibu kilomita 400 Mashariki mwa Moscow.