KOREA KASKAZINI-USALAMA

Korea Kaskazini yajiandaa kwa gwaride kubwa la kijeshi Jumamosi, licha ya tishio la kiafya

Korea Kaskazini: gwaride kubwa la jeshi linalotarajiwa huko Pyongyang licha ya tishio la kiafya
Korea Kaskazini: gwaride kubwa la jeshi linalotarajiwa huko Pyongyang licha ya tishio la kiafya AFP

Korea Kaskazini inaandaa gwaride kubwa la kijeshi ambalo leo Jumamosi kuadhimisha miaka 75 tangu kundwa kwa chama tawala cha Labour Party, licha ya tishio la kiafya kutokana na janga la COVID-19.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Pyongyang inasadikiwa kuwa in inaweza kuonyesha makombora mapya ya masafa marefu na Kim Jong-un kulihutubia taifa, kulingana na habari kutoka vyombo vya habari kadhaa na maafisa nchini Korea kaskazini.

Vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini, wiki hii, vilichapisha picha zinazoonyesha umati wa wajumbe na wageni wengine waliovaa barakoa wakiwasili katika mji mkuu wa nchi hiyo kuhudhuria sherehe hizo.

Shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap limenukuu vyanzo visivyo rasmi ambavyo vilionyesha ishara kwamba televisheni ya serikali ya Korea Kaskazini imekuwa ikiandaa kutangaza gwaride. Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un pia anaweza kutlihutubia taifa, chanzo hiki kimeongeza.

Kulingana na maafisa wa Korea Kusini na Marekani, Korea Kaskazini inaweza kutumia fursa ya gwaride hili kuonyesha kombora lake jipya la masafa marefu.