ARMENIA-AZERBAIJAN-URUSI-USALAMA

Mawaziri wa Mambo ya nje wa Armenia na Azerbaijan wasubiriwa Moscow

Stepanakert, mji mkuu wa Nagorno-Karabakh ukikumbwana mashambulizi mapya ya anga, Oktoba 4, 2020.
Stepanakert, mji mkuu wa Nagorno-Karabakh ukikumbwana mashambulizi mapya ya anga, Oktoba 4, 2020. RFI/ANISSA EL JABRI/BERTRAND HAECKLER

Armenia na Azabajani zimethibitisha kuwasili katika mji mkuu wa Urusi, Moscow, leo Ijumaa kwa mawaziri wao wa Mambo ya Nje kwa mazungumzo kuhusu mzozo wa Nagorno-Karabakh, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Baku na Yerevan wamethibitisha kushiriki katika mazungumzo ya Moscow. Maandalizi yanaendelea vizuri," amesema Maria Zakharova, msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, aliyenukuliwa na shirika la habari la RIA.

Siku ya Alhamisi Kremlin ilimwalika Waziri wa Mambo ya Nje wa Armenia Zohrab Mnatsakanian na mwenzake wa Azerbaijan Jeikhun Bayramova.

Baada ya kusitishwa kwa miaka kadhaa, mzozo kati ya vikosi vya Azerbaijan na wanaharakati wanaotaka kujitenga wa Armenia huko Nagorno-Karabakh ulianza tena Septemba 27 kwa nguvu isiyo na kifani tangu mapigano yaliyofuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti mwaka 1991.