CHINA-CORONA-AFYA

COVID-19: China yawafanyia vipimo wakaazi milioni 6 wa Qingdao baada ya kesi 12 kugunduliwa

China sasa inafanya kampeni za vipimo kwa wengi mara moja, kama vile katika kituo hiki cha upimaji huko Shenyang, Liaoning, kaskazini Mashariki mwa nchi, Julai 29, 2020.
China sasa inafanya kampeni za vipimo kwa wengi mara moja, kama vile katika kituo hiki cha upimaji huko Shenyang, Liaoning, kaskazini Mashariki mwa nchi, Julai 29, 2020. STR / AFP

Katika vita vyake dhidi ya kuibuka tena mlipuko mpya wa virusi vya Corona, China inaendelea na mikakati mbalimbali. Watu wasiopungua milioni 6 wanaendelea kufanyiwa vipimo vya PCR kuanzia Jumatatu hii, Oktoba 12 huko Qindgao katika pwani ya Mashariki mwa nchi.

Matangazo ya kibiashara

Kampeni hiyo ya vipimo inakuja baada ya kugunduliwa kwa visa vitatu vya maambukizi mwishoni mwa wiki hii iliyopita. Na asubuhi ya Jumatatu hii, maafisa wa afya wameripoti visa vipya 12 ambavyo pia vinahusiana na virusi vya Corona katika hospitali moja ya mji wa Qingdao.

Tangu Jumapili jioni, idadi kubwa ya maafisa wa afya na vifaa vingi vimepelekwa katika mji wa Shandong kwa kampeni ya vipimo ambayo itadumu siku tatu.

Mlipuko wa sasa wa virusi vya Corona au COVID-19 viliripotiwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan, nchini China Desemba 31, 2019.

Mji huo ndio kitovu cha ugonjwa wa COVID-19 ambao unasababishwa na virusi vya Corona.