BELARUS-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Polisi wa Belarus ruksa kutumia silaha za moto kukabiliana na waandamanaji

Polisi wa Belarus wapewa amri ya kutumia silaha za moto wakati wa maandamano.
Polisi wa Belarus wapewa amri ya kutumia silaha za moto wakati wa maandamano. REUTERS

Polisi wa Belarus waeruhusiwa kutumia silaha moto wakati wa lazima, na serikali ya Minsk imelaani maandamano yenye msimamo mkali dhidi ya serikali.

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama viliwakamata watu 713 siku ya Jumapili na kutumia maji ya kuwasha na fimbo kuwatawanya waandamanaji wanaotaka uchaguzi mpya wa urais.

Makumi ya maelfu ya raia wa Belarus wamekuwa wakiandamana kila mwishoni mwa wiki tangu kuchaguliwa tena Alexander Lukashenko Agosti 9. Kulingana na upinzani, ameshinda uchaguzi huo baada ya kughushi matokeo ya uchaguzi.

Oktoba 2, Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya maafisa karibu arobaini wa Belarus wanaodaiwa kuhusika katika udanganyifu wa uchaguzi na ukiukaji wa haki za binadamu.

Kwa kujibu, rais wa Belarusi, ambaye Vladimir Putin ndiye mshirika wake mkuu, alitangaza siku hiyo hiyo kwamba alikuwa ameandika orodha ya watu waliopigwa marufuku kuingia katika nchi yake na aliwarejesha nyumbani mabalozi wake waliokuwa nchini Poland na Lithuania.