ARMENIA-AZERBAIJAN-WHO-CORONA-AFYA

WHO: Mapigano Nagorno-Karabakh yasababisha kusambaa kwa Corona

Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki mbili sasa na zaidi ya watu 600 wamepoteza maisha huku wengine, wakisalia bila makwao.
Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki mbili sasa na zaidi ya watu 600 wamepoteza maisha huku wengine, wakisalia bila makwao. Gor Kroyan/REUTERS

Shirika la afya duniani WHO, linaonya kuwa mapigano yanayoendeka kati ya majeshi ya Azerbaijan na Armenia jimbo tata la Nagorno-Karabakh, yanachangia kusambaa kwa maambukizi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea kwa wiki mbili sasa na zaidi ya watu 600 wamepoteza maisha huku wengine, wakisalia bila makwao.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesus, ameaonya kuwa nchi mbalimbali duniani, zinastahili kukaza kambi kuzuia maambukizi hayo.

Watu zaidi ya Milioni 37 wameambukizwa Corona kote duniani huku wengine zaidi ya Milioni Moja wakipoteza maisha.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.