THAILAND-SIASA-USALAMA

Polisi yakabiliana na waandamanaji Bangkok

Maandamano yameshuhudiwa tena katika jiji kuu la Thailand, Bangkok, kupinga kutangazwa kwa hali ya hatari nchini humo na kuzuia mikutano ya watu.

Maandamano hayo yaliyoongozwa na wanafunzi yalizuka baada ya shinikizo kutaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha, mwanajeshi wa zamani aliyechukua madaraka mwaka 2014.
Maandamano hayo yaliyoongozwa na wanafunzi yalizuka baada ya shinikizo kutaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha, mwanajeshi wa zamani aliyechukua madaraka mwaka 2014. REUTERS/Jorge Silva
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji pia wanataka kuachiliwa huru kwa viongozi wa waandamanaji wakiwemo watu wengine 20 waliokamatwa na maafisa wa usalama.

Hali ya hatari ilitangazwa baada ya kuzuka kwa maandamano jijini Bangkong na hatua ya serikali, inapiga marufuku mikutano ya watu zaidi ya wanne.

Maandamano hayo yaliyoongozwa na wanafunzi yalizuka baada ya shinikizo kutaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha, mwanajeshi wa zamani aliyechukua madaraka mwaka 2014.

Aidha, wanataka mageuzi katika wadhifa wa Mfalme Vajira long korn ambaye kwa kipindi kirefu anaishi nje ya nchi.