ARMENIA-AZERBAIJAN-USALAMA

Nagorno-Karabakh: Mapigano yaongezeka, kumi na mbili wauawa Azerbaijan

Mapigano huko Nagorno Karabakh yameongezeka kati ya Azerbaijan wanaharakati waliojitenga nchini Armenia.
Mapigano huko Nagorno Karabakh yameongezeka kati ya Azerbaijan wanaharakati waliojitenga nchini Armenia. AFP

Watu kumi na wawili wameuawa katika shambulio lililotokea Ijumaa usiku katika eneo la makazi huko Gandja, mji wa pili kwa ukubwa nchini Azerbaijan, Mamlaka imesema leo Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano huko Nagorno-Karabakh yameongezeka kati ya Azerbaijan wanaharakati waliojitenga nchini Armenia.

Mapema, mashambulio ya jeshi la Azerbaijan yalilelenga mji mkuu wa eneo lililojitenga la, Stepanakert, kulingana na waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Wakaazi wengi katika mji huo walitoroka makaazi yao tangu kuanza kwa mapigano hayo mnamo Septemba 27.

Shambulizi hili mbaya la Ijumaa usiku huko Ganja lilifuatiwa na shambulizi la pili katika sehemu nyingine ya jiji na kisha risasi zilizolenga mji jirani wa Mingecevir.

Mashambulizi haya ya anga, pamoja na mapigano kwenye maeneo ya vita, vinaonyesha kushindwa kwa jamii ya kimataifa kwa wiki tatu kusuluhisha mgogoro huo.

Ijumaa jioni Mkuu wa Pentagon Mark Esper na Waziri wa majeshi wa Ufaransa Florence Parly walisisitiza juu ya haja ya kumaliza uhasama huo.