BELARUS-SIASA-USALAMA

Belarus: Upinzani waapa kuingia mitaani licha ya tishio la risasi za moto

Jumapili iliyopita, maandamano ya kila wiki huko Minsk yalivunjwa kikatili na polisi, ambayo ilitumia mizinga ya maji na mabomu dhidi ya umati wa waandamanaji na kuwakamata mamia ya watu.
Jumapili iliyopita, maandamano ya kila wiki huko Minsk yalivunjwa kikatili na polisi, ambayo ilitumia mizinga ya maji na mabomu dhidi ya umati wa waandamanaji na kuwakamata mamia ya watu. AFP

Upinzani wa Belarus unatarajia kufanya maandamano mengine makubwa leo Jumapili dhidi ya rais Alexander Lukashenko, licha ya kutishiwa kupigwa risasi za moto na polisi, ambayo ilivunja maandamano ya awali ya Jumapili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya pia yanaonekana kuwa huenda ya yakawa makubwa zaidi na ya kwanza tangu Bwana Lukashenko, aliye madarakani tangu 1994, kupewa onyo na kiongozi wa upinzani Svetlana Tikhanovskaïa, aliye uhamishoni nchini Lithuania.

Svetlana Tikhanovskaïa alitoa muda kwa rais Lukashenko hadi Oktoba 25 awe amekwisha ondoka madarakani, vinginevyo atatoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuingia mitaani na kufanya mgomo wa jumla.

Rais Alexander Lukashenko, mwenye umri wa miaka 66, ambaye anaendelea kukabiliwa na shinikizo lisilokuwa la kawaida tangu uchaguzi wa urais wenye utata wa Agosti 9, hajaonyesha nia ya kuzingatia madai ya wapinzani wake.

Viongozi wa upinzani muhimu wa Belarus sasa wamefungwa na baadhi wamekimbilia z uhamishoni, nje ya nchi. Jumapili iliyopita, maandamano ya kila wiki huko Minsk yalivunjwa kikatili na polisi, ambayo ilitumia mizinga ya maji na mabomu dhidi ya umati wa waandamanaji na kuwakamata mamia ya watu.