MAREKANI-JAPAN-AUSTRALIA-CHINA-USALAMA

Bahari ya China: Marekani, Japan na Australia wafanya mazoezi ya kijeshi

Marekani na washirika wake wanaendelea kutoa wito wa uhuru wa kusafiri katika Bahari ya Kusini mwa China, licha ya madai ya Beijing kuwa eneo hilo ni sehemu yake ya ardhi.
Marekani na washirika wake wanaendelea kutoa wito wa uhuru wa kusafiri katika Bahari ya Kusini mwa China, licha ya madai ya Beijing kuwa eneo hilo ni sehemu yake ya ardhi. REUTERS

Majeshi ya Marekani, Japani na Australia wamefanya mazoezi ya kijeshi katika Bahari ya Kusini mwa China Jumatatu, kikosi cha wanamaji cha Marekani kimetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni mazoezi yao ya tano ya pamoja katika mwaka huu katika eneo hili, kikosi hicho cha jeshi ma Marekani kimesema katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne.

Marekani na washirika wake wanaendelea kutoa wito wa uhuru wa kusafiri katika Bahari ya Kusini mwa China, licha ya madai ya Beijing kuwa eneo hilo ni sehemu yake ya ardhi.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa China alisema kuwa, Bahari ya China Kusini ni 'nyumba ya pamoja' ya China na nchi za Kusini Mashariki mwa Asia na hivyo nchi za eneo hilo zinapaswa kuchukua hatua za amani na ustawi.

Kwa miaka kadhaa sasa, Marekani imekuwa ikiibua vita vya kisaikolojia dhidi ya China katika Bahari ya China Kusini kwa kutumia mbinu mbali mbali.

Kulingana na wadadisi Marekani inatekeleza sera za kuibua mahasimu wa China miongoni mwa nchi zinazopakana na nchi hiyo na wakati huo huo kuchukua hatua kali za upande mmoja dhidi ya Beijing.