INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya chini zaidi ya maambukizi ya kila siku yathibitishwa India

Wataalam wana hofu ya kuongezeka kwa idadi ya visa vya maambukizi wakati huu zinakaribia sherehe za Wahindu kutoka jamii ya Durga Puja na Diwali, ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba na katikati ya mwezi wa Novemba, mtawaliwa.
Wataalam wana hofu ya kuongezeka kwa idadi ya visa vya maambukizi wakati huu zinakaribia sherehe za Wahindu kutoka jamii ya Durga Puja na Diwali, ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba na katikati ya mwezi wa Novemba, mtawaliwa. REUTERS

India Jumanne imerekodi idadi ya chini zaidi ya kila siku ya maambukizi ya virusi vya Corona tangu miezi minne iliyopita, baada ya visa vipya 46,790 kuthibitishwa.

Matangazo ya kibiashara

Jumla ya visa tangu kuzuka kwa janga hilo sasa vimefikia watu milioni 7.6 walioambukizwa virusi hivyo, na kuifanya kuwa nchi ya pili iliyoathirika zaidi baada ya Marekani, kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya. Kuhusu vifo, watu 587 wameripotiwa kufariki dunia leo Jumannei, na kufanya idadi ya waliofariki dunia kufikia 115,197 nchini humo.

Wataalam wana hofu ya kuongezeka kwa idadi ya visa vya maambukizi wakati huu zinakaribia sherehe za Wahindu kutoka jamii ya Durga Puja na Diwali, ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba na katikati ya mwezi wa Novemba, mtawaliwa.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.