India yamwachilia askari wa China aliyevuka mpaka wa Himalaya
Imechapishwa:
Mwanajeshi wa China ambaye alikamatwa na jeshi la India wiki hii baada ya kuvuka eneo la mpaka linalozozaniwa la Himalaya kati ya nchi hizo mbili amerudishwa China Jumanne jioni, chanzo cha serikali huko New Delhi kimebaini.
Awali jeshi la India llisema lilimkamata askari wa China Jumatatu katika eneo la mashariki mwa Ladakh.
Huko Beijing, gazeti rasmi la Jeshi la Ukombozi wa Watu limeripoti kwamba askari huyo amerejea China asubuhi na mapema siku ya Jumatano.
China na India zilitangaza mwezi uliopita makubaliano ya kusitisha uhasama kwenye eneo la mpaka la Himalaya.
Maelfu ya wanajeshi kutoka nchi zote mbili wametumwa katika eneo hilo baada ya mapigano mabaya ya mwezi Juni.