ARMENIA-AZERBAIJAN--USALAMA

Baku na Yerevan washutumiana kwa kukiuka makubaliano ya usitishaji vita Nagorno-Karabakh

Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh, Septemba 28, 2020.
Mapigano kati ya Armenia na Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh, Septemba 28, 2020. KAREN MINASYAN / AFP

Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan imesema leo Jumatatu kwamba wanajeshi wa Armenia wamekiuka makubaliano ya usitishaji mapigano ulifikiwa Jumapili Oktoba 25, watekeleza mashambulizi katika vijiji vya Terter na Lachin.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni "habari isiyo sahihi," imebaini wizara ya ulinzi ya Nagorno-Karabakh, ikilaumu jeshi la Azerbaijan kwa kufanya shambulio la kombora dhidi ya ngome zake za jeshi la Armenia, Kaskazini Mashariki mwa eneo la mawasiliano.

Marekani ilitangaza Jumapili kwamba makubaliano mapya ya kibinadamu yataanza kutekelezwa huko Nagorno-Karabakh leo Jumatatu alaasiri, licha ya mapigano zaidi Jumapili mchana.

Awali katika taarifa ya pamoja, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani na serikali ya Azerbaijan na Armenia zilibaini kwamba mkataba wa kusitisha mapigano utaanza kutukelezwa leo Jumatatu asubuhi saa 8:00.