URUSI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Vifo 346 vyathibitishwa nchini Urusi

Urusi imerekodi leo Jumatano visa vipya 16,202 vya maambukizi ya virusi vya Corona na idadi kubwa ya vifo 346 kwa nchi hiyo katika muda wa saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya waliofariki dunia kutokana na virusi hivyo kufikia 26,935.

dadi ya visa vya maambukizi nchini Urusi, ambayo ina wakaazi karibu milioni 145, imefikia 1,563,976, na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi ya nne ulimwenguni iliyoathirika zaidi na janga hilo.
dadi ya visa vya maambukizi nchini Urusi, ambayo ina wakaazi karibu milioni 145, imefikia 1,563,976, na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi ya nne ulimwenguni iliyoathirika zaidi na janga hilo. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya visa vya maambukizi nchini Urusi, ambayo ina wakaazi karibu milioni 145, imefikia 1,563,976, na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi ya nne ulimwenguni iliyoathirika zaidi na janga hilo.

Hayo yanajiri wakati Tume ya Ulaya imependekeza mfululizo wa hatua mpya dhidi ya janga la COVID-19 katika bara la Ulaya kutokana na ongezeko la maambukizi mapya, ukitolea wito nchi 27 wanachama wa Umoja huo kuboresha uratibu wao.

Ujerumani, ambayo ilichapisha viwango vya chini vya maambukizo kuliko nchi zingine kubwa wakati wa mlipuko wa kwanza wa janga hilo, sasa inakabiliwa na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya kesi mpya: takwimu zilizotolewa Jumatano zinaonyesha visa vipya 14,964 vya maambukizi katika muda wa saa 24, na kufanya idadi ya visa vya maambukizi kufikia 464,239, na vifo vifo 85 vya nyongeza.

Ongezeko la maambukizi mapya limeendelea kuripotiwa katika nchi mbalimbali barani Ulaya, katika baadhi ya nchi za Amerika na Asia.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.