INDIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: India yarekodi zaidi ya visa milioni 8 vya maambukizi

Kwa idadi ya visa vya maambukizi, India inaendelea kuwa nyuma ya Marekani (milioni 8.8), katika orodha ya nchi zilizoathirika zaidi na janga hilo.
Kwa idadi ya visa vya maambukizi, India inaendelea kuwa nyuma ya Marekani (milioni 8.8), katika orodha ya nchi zilizoathirika zaidi na janga hilo. REUTERS/Rupak De Chowdhuri

Visa zaidi ya milioni 8 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimethibitishwa nchini India leo Alhamisi, baada ya visa vipya 49,881 kuripotiwa katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, kulingana na takwimu ziliztolewa na Wizara ya Afya.

Matangazo ya kibiashara

Kwa idadi ya visa vya maambukizi, India inaendelea kuwa nyuma ya Marekani (milioni 8.8), katika orodha ya nchi zilizoathirika zaidi na janga hilo.

Idadi ya visa vya kila siku vya maambukizi vimepungua hivi karibuni lakini wataalam wanahofu kuanza tena kusambaa kwa virusi hivyo baada ya kuingia kwa kipindi cha sherehe kuu za dini la Kihindu.

Idadi ya vifo vinavyotokana na Corona nchini India imeongezeka kutoka 517 katika muda wa saa 24 hadi 120,527, wizara imeongeza.