CHINA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Visa vipya 47 vyaripotiwa China

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019. Hector RETAMAL / AFP

China imerekodi visa vipya 47 vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, ikiwa ni idadi ya juu zaidi tangu miezi miwili iliyopita, Tume ya Kitaifa ya Afya imebaini leo Alhamisi katika mkutano wake wa kila siku kuhusu janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kati ya kesi hizo mpya, 23 ni maambukizi mapya katika jiji la Kashgar ambalo libapatikana katika mkoa wa Xinjiang, Kaskazini Magharibi mwa China. Kesi zingine zilizoripotiwa zote ni kutoka nje.

Kulingana na takwimu hizi, visa 85,915 vya maambukizi vimethibitishwa katika China bara.

Janga la Corona limesababisha vifo vya watu 4,634 nchini China. Hakuna vifo vipya vilivyoripotiwa leo Alhamisi.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.